“Nilimtahadharisha Mbasha mapema na kumwambia hizo anko ziishie kwenye instagram na ujumbe kaupata maana siku hizi mtu akimuita mwanao anko muangalie mara mbilimbili anaweza kumsababishia madhara baadaye,” Monalisa ameiambia Globalpublishers ni baada ya kuulizwa akionekana hataki mchezo mchezo kwa binti yake huyo aliyebukua division 1 kidato cha nne .
.
Issue ilivyoanza, Monalisa alitupia picha ya mtoto wake Sonia kwenye Instagram akikata keki kwa niaba yake mara akatokea Mbasha na kutupia komenti ‘ankooo huyo’ akarudishiwa jibu na Mona ‘hiyo anko vipi baba’.