Imepita miaka 11 sasa tangu Dunia ya muziki wa HipHop ishuhudie Beef kali kati ya Rapa Rick Ross na 50 Cent.


Beef hilo limeonekana kuoendelea tena baada ya Rick Ross kumzungumzia 50 Cent na kusema kuwa amefulia sio kama alivyokuwa zamani.

Rick Ross amesema hayo katika kipindi cha BigBoy wakati alipoenda kutangaza ujio wa Album yake mpya ya “Port Of Miami II” ambayo itaachiwa August 9 Mwaka huu, na amesema yupo tayari kumaliza Beef lake na 50 Cent kama atakuwa na thamani,

“Mimi ni Mfanyabiashara kama 50 Cent ana thamani kama alivyokuwa nayo mwanzo nipo tayari kumaliza hili suala. Hii sio utani jamaa kwa sasa amefulia, kipindi kile ukipita mitaa ya Jiji la Los Angeles lazima uwasikilize tu 50 Cent na The Game iwe unawapenda au unawachukia” amesema Rick Ross.

Aidha rapa huyo aliendelea kusema kwa sasa hivi yupo vizuri, na kama 50 Cent anataka wamalize tofauti zao basi ajitahidi afanye vizuri kama alivyofanya miaka 8 iliyopita.

Tofauti za wawili hao zilianza mwaka 2008 na walifika hatua hadi za kushambuliana kwa kupigana Risasi miaka kadhaa iliyopita.