Mwanamama Zari The Boss Lady huwa hataki kupitwa na kila fursa inayokatisha mbele yake, hasa linapokuja suala la kuingiza mkwanja.

Mwanamama huyo amefanikiwa kupata dili la kuwa Jaji kwa mara ya pili na pia ametajwa kuwa mlezi kwenye shindano la kumtafuta Miss Uganda2019, ambapo mwaka jana pia alikuwa Jaji wa shindano hilo.

Kupitia mtandao wa Instagram, waandaaji wa shindano hilo wamethibitisha hilo kwa kuandika: "We are excited to have our judge & patron Zari back.

She will be in Uganda for #MissUganda19 Grandfinale happening on Friday  the 26th of July.” wameongeza.

Shindano hilo linatarajiwa kufanyika Julai 26, Ijumaa hii katika ukumbi wa hoteli ya Kampala Sheraton.