Afisa Masoko wa Mobisol Farid Abdallah (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda na Mkurugenzi wa TANTRADE Edwin Rutageruka walipotembelea banda la Kampuni ya Mobisol katika maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
 Wananchi wakipata maelezo kutoka kwa watoa huduma ya kampuni ya Mobisol waliopo jengo la Karume Hall katika maonesho ya ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda ametoa pongezi kwa kampuni ya Mobisol kwa juhudi wanazozifanya kwa kusambaza nishati ya nguvu ya jua (solar power) nchi nzima.

Pinda amesema hayo leo alipotembelea banda la Kampuni hiyo liliopo ndani ya Karume Hall wakishiriki maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika banda hilo, Pinda amepata maelekezo mbalimbali kuhusiana na vifaa vinavyotumia nishati jmya nguvu ya jua na namna vinavyofanya kazi kwenye Televisheni, Jokofu na hata feni ambazo vyote vinapatikana kwao.

Meneja masoko wa Mobisol, Seph Materu amesema kuwa kampuni yao imesambaa nchi nzima isipokuwa Mtwara ila wapo mbioni kuweka tawi lao kwenye Mkoa huo.

Materu amesema, watanzania wengi wanaamini kuwa solar ni kwa ajili ya kuwasha taa tu ila inafanya kazi kubwa sana ikiwemo kuwasha televisheni, majokofu na hata vifaa vingine vya umeme.

Amesema kampuni yao imekuwa inasambaza umeme huo kwenye mikoa mbalimbali ila changamoto kubwa ni elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya nishati hiyo ila wamekuwa wanaelewa na kuanza kutumia bidhaa za mobisol.

Aidha, kampuni ya Mobisol ina solar kubwa zinazoweza kuwasha hospital, mashuleni pia wanauza bidhaa zao kwa kulipa kidogo kidogo na kuwataka wananchi watembelee banda lao na kujionea namna nishati jua inavyofanya kazi.

Kampuni ya Mobisol ipo nchini toka mwaka 2015 na imejizatiti kuondoa kero ya umeme kwa wananchi wa mjini na vijijini kote nchini.