Sakata la kutoweka kwa Azory Gwanda hatimaye kumechukua sura mpya baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi,  kusema kwamba mwandishi huyo si pekee aliyetoweka na kufariki katika eneo la Rufiji.

“Tatizo la Rufiji ni moja ya matukio yaliyoumiza na kusikitisha ambayo Tanzania tumeyapitia, pale Rufiji sio Azory Gwanda pekee ambaye amepotea na kufariki, nikuhakikishie tunachukua kila hatua, ili watu wetu wawe salama awe Mwanahabari, Polisi au raia wa kawaida” Waziri Kabudi

“Katika eneo la Rufiji sio tu Azory Gwanda aliyetoweka na kufariki, nataka kukuhakikishia kwamba tunachukua kila hatua sio tu katika eneo la Rufiji bali maeneo mengine ya Tanzania ili kuhakikisha kuwa watu wetu wako salama-sio tu waandishi”- Waziri Kabudi