Meneja wa Banda la Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Shaaban Kiulah akizungumza na mwaahabari mara bbaad ya kutembelea banda katika maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es salaam.
Wananchi wakitapa maelezo katika banda la Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) lililopo maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Zainab Nyamka na Cathbert Kajuna, Globu ya Jamii.

Watanzania waaswa kutembelea Misitu ya hifadhi ya mazingira asilia ili kujionea tunu ya vivutio vya utalii ambavyo Tanzania imebarikiwa.

Akizungumza na Michuzi Blog, Meneja wa Banda la Wakala wa Misitu Nchini (TFS) Shaaban Kiulah amesema kuna misitu ya asili ambapo kuna vivutio vingi vya asili na baadhi havipatikani sehemu yoyote duniani.

Ameyasema hayo katika maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es salaam.

Kiulah amesema, TFS ni wakala wa serikali wakisimamia hifadhi na misitu ambapo kuna misitu ya asili na ile ya kupanda (mashamba) inayofikia 24 nchi nzima.

Amesema, katika shughuli wanazozifanya ikiwemo utalii kwenye hifadhi, wanashughulika na ufugaji wa nyuki na uvunaji wa mbao.

Kiulah ameeleza kuwa, kwenye maonesho hayo wapo wadau 53 wote wanaotumia mazao ya miti ambapo wamegawanyika katika makundi tofauti yakiwemo wa wachonga vinyago, mazao ya nyuki (asali), mazao ya siti mbao, nishati mbadala na tiba asilia.

Amesema makundi hayo yote kwa pamoja yanashirikiana na TFS na sekta binafsi kutoa ushauri na elimu kwa wananchi kuhusiana na umuhimu wa kutunza misitu na hifadhi kwa manufaa ya nchi.

Aidha, amewataka wanachi watunze, walinde na kutumia rasilimali kwa njia endelevu.

Kiulah amewataka wananchi kujitokeza kwenye banda lao lililopo ndani ya Banda la Maliasili na Utalii kwenda kujifunza na kupata elimu ya masuala mbalimbali na kuoneshwa vivutio vinavyopatikana katkka hifadhi za misitu ikiwemo Hifadhi ya mazingira Magamba.