.Kamishna wa Uraia na Pasipoti Uhamiaji, Gerald Kihinga amesema kuwa Mwandishi wa habari, Erick Kabendera aliyedaiwa kutoweka nyumbani kwake idara ya uhamiaji wanae na wanaendelea kumhoji utata wa uraia wake.

Kamishna Kihinga amesema kuwa Uhamiaji walipata taarifa kutoka kwa wasamalia wema kufuatia utata wa uraia bwana Erick Kabendera.

"Uhamiaji tulipata taarifa kutoka kwa wasamalia wema kufuatia utata wa uraia wa bwana Erick Kabendera baada ya idara kupewa tarifa hizo tulianza kuzifanyia kazi hata hivyo Kabendera mwenyewe hajawahi kuhojiwa kulingana na Uraia wake kwakuwa hakufika katika ofisi ya uhamiaji pamoja na kutumiwa wito mara nyingi lakini hakuweza kufika, " amesema Kamishna Kihinga.

"Uhamiaji kushirikiana na jeshi la Polisi tuliweza kumtafuta na kumpata na mpaka tunavyoongea hivi bwana Kabendera tunae sisi uhamiaji kwaajili ya kumhoji kuhusu utata wa uraia wake."