Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania imeungana na Taasisi ya kimataifa ya Girl Effect kuzindua ‘Tujibebe’ huduma mpya inayotoa elimu ya maisha kupitia simu ikiwalenga vijana waliopevuka wenye umri kati ya 15-19.

Huduma ya Tujibebe itawaunganisha vijana wenye uzoefu katika ujasiriamali kuwahamasisha vijana wengine na kusaidiana kutatua changamoto za maisha huku wakitimiza malengo yao. Maudhui ya tujibebe yanalenga katika kuwapa vijana wa kitanzania taarifa na rasilmali wanazohitaji kufanya maamuzi sahihi ya maisha yao – mafunzo ya kuboresha ujuzi wao, kuanzisha biashara na kusimamia fedha zao. Tujibebe itatumia tovuti pamoja na huduma za simu za IVR kutoa mafunzo kupitia simulizi ya sauti ambayo ni bure kabisa kupitia mtandao wa Vodacom.

Jukwaa la Tujibebe limezinduliwa rasmi na Mjumbe wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) Simon Shayo na wadau mbali mbali wa sekta ya maendeleo, katika hafla iliyofanyika hoteli ya Golden Tulip. Wageni waalikwa walipata nafasi ya kusikia baadhi ya maudhui kutoka kwa watafiti wa Technology Enabled Girl Ambassadors (TEGAs) ambao ndio kiini cha taarifa na maudhui yaliyotumiwa kuhakikisha kwamba Tujibebe inakidhi mahitaji ya wasichana na vijana wa kitanzania.

Akizungumza katika hafla hiyo Bw Shayo  alisema amefurahi kwamba makampuni mengi yanaungana ili kuhakikisha usawa wa kijinsia unaongezeka na pia kuwawezesha vijana kiuchumi, alizipongeza taasisi za Vodacom Tanzania Foundation na Girl Effect kwa kuwekeza katika vumbuzi zinazosaidia kubadilisha maisha ya watu wengi.

 “Tujibebe inaonesha umuhimu wa taasisi binafsi na zile zisizofanya kazi kwa faida kuungana na kuhakikisha malengo endelevu ya maendeleo yanatimia, ninapenda kuzihamasisha taaisis nyingine nyingi Zaidi kuwa wabunifu katika maeneo yao na kuungana na taasisi zingine ili kubuni miradi ambayo itabadilisha maisha ya jamii zinazowazunguka,” aliongeza Shayo 

Serikali inafanya kazi na taasisi mbali mbali ikiwemo UNDP, USAID na Vodacom Tanzania Foundation katika masuala ya kuleta usawa na kuwawezesha wasichana, pia aliwapongeza Vodacom na Girl Effect kwa kuwekeza katika miradi ya maendeleo nchini. “Inabidi wote tushirikiane kuinua vijana wetu na hasa wasichana kwani wao ndio Tanzania ya baadae. Napenda kuwasihi wadau kuungana pamoja kutengeneza miradi kwa ajili ya kuwasaidia vijana wengi zaidi.” aliongeza Shayo.

“Sote tunafahamu kwamba teknolojia ya simu ina uwezo wa kubadilisha dunia, tunafuraha sana kuungana na Girl Effect, kupitia mtandao wetu ambapo tutaweza kuwafikia vijana wengi zaidi na kuwafanya wafikie malengo yao” alisema Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia.
Akielezea faida za jukwaa la Tujibebe katika kuleta mabadiliko katika maisha ya Vijana wa Kitanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa Girl Effect, Jessica Posner Odede alisema maudhui ya tujibebe yametengenezwa kwa ajili ya kuwaunganisha vijana wote lakini lengo kubwa ni kubadilisha maisha ya wasichana watakaotumia elimu kutoka Tujibebe.

 “Mara nyingi vijana huwa na maswali mengi kuhusiana na kesho yao, na hawajui mahali pakupata majibu sahihi – kuanzia kuwa na ujuzi kwa ajili ya kupata kazi, jinsi ya kupata pesam na pia namna ya kutunza pesa hizo. Hapo zamani ilikuwa ni vigumu kwa wasichana kupata taaarifa hizi - leo tunazindua tujibebe ili wakiingia kwenye mtandao wapate elimu mtandaoni, sio tu wapakue mambo ya kufurahisha, bali pia waweze kupata mafunzo ambayo yanagusa maisha yao ya kila siku. Lengo letu kubwa ni kutumia tujibebe kuwaunganisha wasichana na huduma zinazowazunguka na kutengeneza mabadiliko ya kudumu.

Mwezi uliopita Vodacom Tanzania Foundation ilizindua mpango mkakati wa miaka mitatu 2019-2021 ambao umelenga kuleta maendeleo jumuishi katika afya, elimu na mazingira. Kimataifa Vodafone Foundation ni mbia wa Girl Effect katika kubuni miradi mbali mbali ya kuwawezesha vijana kutumia teknolojia ya simu.
 Mjumbe wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) Simon Shayo akizungumza wakati wa  kuzindua ‘Tujibebe’ huduma mpya inayotoa elimu ya maisha kupitia simu ikiwalenga vijana waliopevuka wenye umri kati ya 15-19 iliyowezeshwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania pamoja na Taasisi ya kimataifa ya Girl Effect.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vodacom, Hisham Hendi akizungumzia mchango wa Taasisi ya Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania inavyoshiriki kuinua watoto wa kike wakati wa uzinduzi wa Tujibebe’ huduma mpya inayotoa elimu ya maisha kupitia simu ikiwalenga vijana waliopevuka wenye umri kati ya 15-19. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Juma Nkamia akizungumza kuhusu wabunge wanavyoishauri serikali kwenye ulinzi wa mtoto wa kike ili waweze kufikia malengo yao wakati wa uzinduzi wa ‘Tujibebe’ huduma mpya inayotoa elimu ya maisha kupitia simu ikiwalenga vijana waliopevuka wenye umri kati ya 15-19.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya kimataifa ya Girl Effect, Jessica Posner Odede akizungumza kuhusu namna taasisi hiyo ilivyojikita  kutoa huduma mpya inayotoa elimu ya maisha kupitia simu ikiwalenga vijana waliopevuka wenye umri kati ya 15-19 ijulikanayo kama ‘Tujibebe’.
Msheheleshaji Tulanana Bohela akifanya mahojiano na vijana waliofikiwa na  Taasisi ya kimataifa ya Girl Effect kupitia ‘Tujibebe’ huduma mpya inayotoa elimu ya maisha kupitia simu ikiwalenga vijana waliopevuka wenye umri kati ya 15-19 iliyowezeshwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania pamoja na Taasisi ya kimataifa ya Girl Effect.
Baadhi ya Viongozi, Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na vijana wakifuatilia uzinduzi wa ‘Tujibebe’ huduma mpya inayotoa elimu ya maisha kupitia simu ikiwalenga vijana waliopevuka wenye umri kati ya 15-19 iliyowezeshwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania pamoja na Taasisi ya kimataifa ya Girl Effect.