Bi. Olive Njoroge (wapili kushoto) na Bw. Paul Muhato, wakimzawadia mteja vocha ya manunuzi kwenye kituo cha Engen Msasani Julai 26, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa VISA Tanzania, Bi. Olive Njoroge (kushoto), akipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa Engen Tanzania, Bw. Paul Muhato wakati wa uzinduzi wa kampeni ya miezi miwili ya kuhamasisha watumiaji wa mfumo wa kufanya malipo kupitia simu ya mkononi (Visa-on-mobile) na malipo mengine ya kidijitali ambapo kampuni hizo mbili zimeanzisha ushirikiano ili kuendeleza matumizi ya malipo kwa njia hiyo. Kampeni hiyo ilizinduliwa kwenye kituo chga mafuta Engen kilichoko eneo la Msasani jijini Dar es Salaam Julai 26, 2019.
Bi. Olive Njoroge (kushoto) na Bw. Paul Muhato, wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Julai 26, 2019.
Bw. Paul Muhato(kulia) na Bi. Olive Njoroge, wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Julai 26, 2019.
Kampeni hiyo imeanza leo Ijumaa Julai 26, 2019 na wateja ambao watanunua mafuta yenye thamani ya shilingi elfu 50,000/= siku za Ijumaa na Jumapili wakitumia Visa on mobile au kutumia kadi za benki yenye nembo ya VISA wataweza kupata zawadi mbalimbali kupitia ushirikiano huu baina ya VISA na Engen Petrol Stations.
KAMPUNI ya malipo ya kidigitali VISA na ile ya kuuza mafuta, Engen Tanzania wamezindua kampeni ya miezi miwili kuanzia leo Ijumaa Julai 26, 2019 yenye lengo la kuhamasisha utumiaji wa mfumo wa kufanya malipo kupitia simu ya mkononi (Visa-on-mobile), na malipo mengine ya kidijitali wakati wa malipo wakiwa kwenye vituo vya Engine nchi nzima.

Wateja ambao watanunua mafuta yenye thamani ya shilingi elfu 50,000/= siku za Ijumaa na Jumapili wakitumia Visa on mobile au kutumia kadi za benki yenye nembo ya VISA wataweza kupata zawadi mbalimbali kupitia ushirikiano huu baina ya VISA na Engen Petrol Stations.

Akizungumza wakati wa uzinduzi humo Mkurugenzi Mkuu wa VISA nchini Tanzania, Bi. Olive Njoroge amesema “Promosheni hii ni nzuri kwa wateja ambao wataweza kufurahia usalama na uzuri wakitumia mfumo wa Visa on mobile na pia wataweza kupata zawadi mbalimbali kupitia ubia wetu na Engen Tanzania.” Alisema Bi. Njoroge wakati w amkutano w apamoja na waandishi wa habari akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Engen Tanzania Bw. Paul Muhato.

Kwa upande wake Mkuurgenzi Mkuu wa Engen Tanzania, Bw. Paul Muhato alisema mara nyngi madereva wa vyombo vya moto hufanya malipo kwa pesa taslimu (cash), wakinunua mafuta ya petrol na dizeli na wakati mwingine mteja anahitaji kwenda kwenye ATM, mchakato ambao huchukua muda mrefu, lakini ukitumia mfumo huu wa Visa on mobile (kufanya malipo kupitia simu ya mkononi (Visa on mobile) ni salama zaidi na huokoa muda, tumefurahi kushirikiana na Visa tukiwahamasisha wateja wetu kutumia mfumo wa malipo kwa njia ya kidijitali na pia kuwapatia zawadi.” Alifafanua Bw. Muhato.