Kiungo wa Harambee Stars na Tottenham Hotspurs ya Uingereza, Victor Wanyama amemkaribisha rasmi nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta katika Ligi Kuu ya Uingereza msimu ujao.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Samatta aliandika: “Ilikuwa ni nafasi nzuri kucheza na mmoja wa wachezaji bora na wa mfano wa kuigwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, tunajivunia uwepo wako ndani ya East Africa (Afrika Mashariki)”.

Naye Victor Wanyama akajibu hilo kwa kusema, 'Nashukuru Sana Kaka yangu,na ni matarajio yangu kukuona Premier League msimu ujao tuendelee kupeperusha bendera ya East Africa".