Malkia wa Bongo Fleva kwa sasa, Vanessa Mdee ameonekana akimrushia maneno aliyekuwa shemeji yake wa zamani Cyrill Kamikaze.


Wawili hao kwa sasa wamekuwa hawana mawasiliano mazuri baada ya kuvunjika kwa penzi la Jux na Vanessa, ambapo hadi sasa kila mtu amemu-unfollow mwenzake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Vanessa Mdee amesema sababu za kumu-unfollow Cyrill Kamikaze kwenye mtandao huo ni kutokana na maneno ambayo aliyaandika katika moja ya post zake baada ya kuachana na Jux, ambayo hakuyapenda.

“Kuna kitu alipost alinikera, sipendi mwanaume ambaye anatabia za kike Kuna post na maneno alikuwa anazungumza sikuyapenda kwahiyo nikamu-unfollow”, amesema Vanessa.

Cyrill Kamikaze aliwahi kusema kwa sasa akiambiwa achague kati ya Vanessa Mdee na Mpenzi mpya wa Jux aitwaye Nnayika, atamchagua Nnayika kwa sababu rafiki yake ndio yupo nae kwa sasa na wala hawezi kumpinga Jux kwenye uamuzi wake.