Acha kabisa! Mfanyabiashara anayemiliki duka la Lin Collection lililopo Sinza, Afrika-Sana jijini Dar, Lilian Pascal amempigia saluti staa wa sinema za Kibongo, Irene Uwoya kwa kumjazia watu.  Lilian ameliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, Uwoya ni mteja wake mkubwa na kitendo chake cha kununua vitu dukani kwake na kupiga picha kisha kutupia mtandaoni kimesababisha watu kujaa dukani kwake.

“Sijui nisemeje kuhusu Uwoya, yaani huwa akinunua kitu kama ni nguo, basi kila mtu anakuja dukani akitaka kitu au nguo kama hiyo na wakijaribu, kuacha ni ngumu sana,” alisema Lilian na kuongeza;“Kwa kweli Uwoya anastahili saluti