Afisa Ubora Maji wa DAWASA Sizya Mongela akitoa maelezo ga ubora wa maji kwa Mteja aliyefika kwenye Banda lao la Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
 Dawati la huduma kwa wateja wakiendelea kutoa huduma kwa wateja waliofika kwenye Banda la Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam DAWASA kwenye Banda lao la Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam. 

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) inawaalika wananchi kutembelea banda lao kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali na kueleza kero zao za majisafi na majitaka. 
---
DAWASA wanashiriki kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam. 

 Katika banda lao, wananchi watafahamu miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mamlaka hiyo na hatua iliyofikia ikiwemo na namna ya kuunganishwa na mtandao wa DAWASA. 

Mbali na hilo, wanatoa maelekezo namna ya kufahamu ubora wa maji na elimu hiyo inatolewa na Afisa ubora wa Maji Sizya Mongela.