Takriban watu 13 wameaga dunia baada ya mvua kubwa kusababisha maporomoko ya ardhi mjini Recife,katika jimbo la Pernambuco kaskazini mashariki mwa Brazil,iongozi wa eneo hilo walisema Jumatano (jana).

Mvua kubwa, iliyoanza kunyesha siku ya Jumanne usiku imesababisha mafuriko,miti kuanguka na maporomoko ya ardhi katika miji kadhaa. Shughuli za uokoaji bado zinaendelea.