JUMA Kaseja, mlinda mlango wa timu ya KMC ambaye ameteuliwa na Kaimu Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Ettiene Ndayiragije kikosi cha timu ya Taifa amesema kuwa watapambana kupata matokeo chanya mbele ya Kenya.

Stars itamenyana na timu ya Kenya, Julai 28 uwanja wa Taifa kwenye michuano ya Chan ambapo jumla ya wachezaji 26 wamechaguliwa na wapo kambini.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kaseja amesema kuwa kitu cha kwanza ni kupambana kwa ajili ya Taifa mengine yatafuata.

"Kazi yetu ni kupambana kwa kuwa ni Taifa moja, imani yetu ni kuona tunapata matokeo chanya kwenye mchezo wetu dhidi ya Kenya.

"Wachezaji tumejipanga na tunajua kwamba mashabiki wanahitaji matokeo chanya hicho ndicho tutakachokifanya," amesema.