Benki ya wakulima kuwafikishia huduma za kifedha kwa wakulima popote pale walipo nchini kupitia benki zao za Ushirika na Kibiashara kupitia mpango wa dhamana ya mikopo. Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) imewapatia wakulima wadogo dhamana ya mkopo yenye thamani ya shilingi billioni moja za kitanzania katika benki ya wananchi Tandahimba (TACOBA).