Meneja Mawasiliano, Bi Chaba Rhuwanya (mwenye miwani kulia) akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo (wa pili meza kuu) wakati wa hafla ya utoaji tuzo iliyotolewana PPRA ya mnunuzi bora kwa mwaka 2017/2018.
Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania, imepokea kwa furaha kubwa tuzo iliyotolewana PPRA ya mnunuzi bora kwa mwaka 2017/2018.

Akipokea tuzo hiyo Meneja mawasiliano, Bi Chaba Rhuwanya ambaye amepokea tuzo hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TADB bwana Japhet Justine amesema wameipokea tuzo hiyo kwa fahari sana, kwa sababu tuzo hiyo nikielelezo cha uongozi bora na usimamizi mzuri wa fedha za umma kwa kuziba mianya ya upotevu wa fedha katika manunuzi.

Amesema usimamizi huo mzuri ndio unaowezesha Benki ya Maendeleo ya Kilimo kuweza kutoa huduma kwa wadau wetu wakubwa ambao ni Wakulima, Wafugaji, na wavuvi na walioko kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo ikiwemo wenye viwanda.

"Ni ahadi yetu kuwa tutaendelea usimamizi mzuri katika manunuzi yetu ili fedha ziweze kuendeleza na kuleta mapinduzi ya kilimo nchini. Sisi Benki ya Maendeleo ya Kilimo tunaamini Kilimo Kinabenkika," amesema Bi. Ryuwanya.