Msanii wa muziki wa kizazi hapa nchini Baraka the Prince, amenyoosha maelezo juu ya suala la yeye kushuka kimuziki, na suala zima la mahusiano yake na Naj.

Baraka the prince amesema hayo leo kupitia EATV&EARadio Digital, baada ya mashabiki zake kusema kwa sasa ameshuka kimuziki.

"Binadamu kaongea, kwani mdomo wa binadamu si upo kwa ajili ya kuongea, hao si mabubu wanaweza kuongea chochote na ndio fikra zao na upeo wao ulipoishia. Mtu kama anaona nimeshuka kimpango wake, mimi pia najua navyoishi kimpango wangu, kama unaona nimeshuka wasanii wapo wengi sio lazima uwe shabiki wa Baraka"

Aidha msanii huyo amezungumzia suala la mahusiano yake kwa sasa na ameweka wazi kuwa hataki kusikia mapenzi  baada ya kuulizwa kuhusu aliyekua mpenzi wake Naj.

"Siwezi kuongelea suala la mahusiano, watu waongee kuhusu kazi zangu, watu waongelee kazi za muziki, kama unataka kuuliza kuhusu Naj mtafute mwenyewe umuulize anaweza akawapa jibu, nina mambo mengi ya kuyaongelea sio mapenzi".

Wawili hao wamezua sintofahamu kubwa kwa kila mmoja baada ya kufutiana picha na kila mtu kumu-unfollow mwenzake katika mtandao wa kijamii wa instagram, hali inayonyesha kutokuwa sawa kwa sasa.