Winga wa kimataifa wa Tanzania Ramadhan Singano, ameweka wazi kuwa kabla ya kujiunga na klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, alifuatwa na Yanga.

Singano amesema hayo kwenye mahojiano na East Africa Television leo Julai 5, 2019 ambapo amesema baada ya kumaliza mkataba na Azam FC, Yanga walimfuata lakini yeye alitaka kwenda nje.

''Mara nyingi nikimaliza mkataba nakwenda kujaribu soka la nje mpaka nikikosa ndio narudi hapa lakini mara hii nimepata TP Mazembe japo mwanzo klabu kama Yanga ilinihitaji lakini nilikuwa nataka kwenda nje'', amesema.

Singano ambaye amewahi kuchezea Simba, amesaini mkataba wa miaka mitano kucheza TP Mazembe ya DR Congo baada ya mkataba wake na Azam FC kumalizika mwezi Juni mwaka huu.