Hata kwa mtutu wa bunduki! Mwigizaji sexy kunako Bongo Movies, Diana Kimari ameweka wazi kuwa hafikirii kufuta tatuu alizochora jina la shoga’ke, Wema Isaac Sepetu.Diana ameliambia Gazeti la Ijumaa  kuwa alimchora kwa moyo wako wote hivyo haoni sababu ya kuzifuta.“Sina mpango wa kufuta tatuu yoyote niliyoandika jina la Wema kwa sababu nilichora kwa mapenzi yangu hivyo acha niendelee kuwa nazo,” alisema Diana ambaye amejichora tatuu mbili za jina la Wema