Tuzo ya “Best Logistics and Transportation Exhibitor” ambayo Shirika la Posta Tanzania limeshinda katika maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba 2019.

Shirika la Posta Tanzania wamenyakua Tuzo ya washindi wa kwanza katika kipengele cha BEST LOGISTICS AND TRASPORTATION EXHIBITOR iliyofanyika katika maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba 2019 iliyotolewa na Makamu wa Raisi Mama Samia Suluhu Hassan wakati akifungua maonyesho hayo.


Baadhi ya wafanyakazi wakishika tuzo waliyoiopata baada ya Shirika kushinda tuzo ya Best Logistics and Transportation Exhibitor.

Maonesho haya ya 43 ya Sabasaba yenye kauli mbiu “ Usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo endelevu ya viwanda” yalianza rasmi Juni 28 na yatamalizika Julai 13 mwaka huu
 ambapo Shirika la Posta Tanzania  ni mmoja wa washiriki kwa mwaka huu.

Unapoingia kwenye Geti kuu la viwanja vya maonesho, Shirika la Posta tupo kwenye barabara ya kwanza kushoto mita chache kutoka geti hilo. Na 1ni jengo la pili kulia unapoingia Geti la mizigo (Geti 2).

Duka la kiamtandao lililoko ndani ya viwanja vya sabasaba. Usajili kwa wafanyabiashara na wenye bidhaa ni bure, kujisajili pitia wesite yetu ya http://bit.ly/2JaETsQ

Huduma zinazotolewa ni kubadisha fedha za kigeni, kusajili bure kwa makampuni, wakulima, wafanyabiashara wakubwa na wadogo, pamoja na sekta ya usafirishaji kujiunga na huduma yetu ya E-commerce na kufanya biashara kupitia mtandao wetu wa Posta online.

Pia wana duka la kubadilishia fedha ndani ya viwanja vya Sabasaba ambapo mteja ataweza kubadili fedha yake ya kigeni ndani ya viwanja.

Wanahuduma ya EMS, kusajili masanduku mapya na huduma ya kulipia masanduku, tunatoa maelezo juu ya huduma yetu mpya ya Posta mlangoni, ambapo mteja anaweza kupelekewa vifurushi na barua zake mpaka mlangoni kupitia wahudumu wetu wa Posta walioko nchi nzima.
 Tunatoa huduma ya posta mlangoni na virtual Box, na kusajili masanduka mapya ya barua.

Watoa huduma wakiwa na nyuso za furaha kukukaribisha katika banda la Shirika la Posta Tanzania ili kuweza kujipatia huduma mbali mbali.