Msanii wa muziki, muigizaji na mjariamali Shilole, amesema anatamani kuwaona mastaa kama Irine Uwoya na Wema Sepetu wakiingia kwenye ndoa.Shishi ambaye yupo katika ndoa kwa mwaka wa pili sasa na mumewe Uchebe, amewataja mastaa hao kupitia mahojiano ya EATV & EA Radio Digital.

"Ndoa mtu hashauriwi anaamua mwenyewe, kama ulivyotafuta mpenzi wa kike na mpenzi wa kiume na ndivyo utakavyoamua kuolewa'', amesema.

Mkali huyo wa Hit kama Nakomaa na Jiji, ameongeza, ''Mimi napenda wasanii wote waingie kwenye ndoa, na natamani Irine Uwoya aingie kwenye ndoa na ataingia tu mimi najua, Wema naye natamani aolewe kwanza wote wanapendeza kwenye ndoa". 

Siku ya jumapili July 7 zilisambaa video mitandaoni zikiwaonyesha Shishi na mumewe Uchebe, wakiwa katika hali ya vurugu  na imeonekana mumewe kumpiga kichwa mlinzi katika moja ya shughuli zilizofanyika hapa jijini Dar es salaam.