Msanii na Mjasiliamali, Shilole amefunguka ishu ya kupigana jana Mlimani City kwenye Birthday ya Mama Diamond na Tanasha.

Shilole amesema hivi "707 was super amazing Nilikuwa na wakati mzuri sana asante san kaka angu Diamonplatnumz kwa kunipa heshima kama wengine wengi waliojumuika pamoja na familiya yako."

"Tukirudi kwenye suala la vile vichwa maana napokea simu nyingi za kutaka kujua kilichotokea jaman naomba niwajibu tu kwa ufupi kwanza niombe Radhi sana kwa WaTanzania na kila ambae suala hili lilimletea usumbufu maana vichwa ni vya kia shwazinega vile."

"By the way tulighafirika kwasababu ya namna tulivyopokelewa aisee tukawa km vibaka tuliovamia shuhuli alafu na kuanza kutaka kumdhalilisha mume wangu mpk kumchania koti for what? Yani nikajikuta tu ule udada mwajuma ukaibuka nikalianzisha vagi."

"Tunashukuru Mungu yaliisha salama tuliyajenga tukaombana radhi. Lkn hii kitu si nzuri, jmn hakuna wasanii wanaotokea shuhuli ya msanii mwenzao bila kualikwa sisi ni familiya unapoenda kwenye jambo la mwenzio ni kushow lov na support hakuna anaekuja kwenye event zangu ukasikia anapata hyo kero mlangoni Kwasabu hakuna kitu kizuri km uandae kitu chako alafu uone watu wako wamekuja kukusupport."

"Haya natumai mmeshapata maelezo nipumzisheni na maswal msije mkala vichwa na nyie.'