Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na Wakuu wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wakipewa maelezo na Mkuu wa kituo cha Kimondo cha Mbozi, Paul Nyelo wakati walipotembelea katika eneo hilo wakati wa kufunga maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani ambapo kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika katika kijiji cha Ndolezi mkoani Songwe.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na wananachi pamoja na wakuu wa mikoa ya Nyanda za juu Kusini waliokuja kushiriki kufunga maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani ambapo kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika katika kijiji cha Ndolezi mkoani Songwe
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila akiwa ameongoza na baadhi ya makatibu tawala waliofika katika viwanja vya Ndolezi mkoani Songwe kwa ajili ya kufunga maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani.
Baadhi ya watumishi wa Idara na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii walioshiriki kwenye maonesho ya siku wakiwa kwenye picha ya pamoja katika banda la Wizara hiyo kabla ya kufunga kwa maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani ambapo kitaifa maadhimisho hayo tyamefanyika mkoani Songwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Nicodemus Mwenga akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Constantine Kanyasu wakati walipokuwa wakitembelea mabanda ya Wajasiliamali katika maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani ambapo kitaifa yamefanyika maadhimisho mkoani Songwe
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akisalimiana na baadhi wananchi na viongozi wa mkoa wa Songwe waliojitokeza kumpokea akiwa mgeni rasmi wa kufunga maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani ambapo kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika mkoani Songwe,.
---
Serikali imeahidi kujenga miundombinu ya kudumu katika Kituo cha Kimondo Mbozi kwa ajili ya maonesho ili kuhamasisha na kukuza utalii kwa mikoa ya Nyanda za juu Kusini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakati alipokuwa akifunga Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu katika kijiji cha Ndolezi mkoani Songwe.
Amesema shabaha ya serikali ya awamu ya tano ni kukuza na kuendeleza Utalii Kusini.
Ametaja miundombinu hiyo itakayojengwa kuwa ni mabanda ya kudumu, viwanja vya michezo, jengo la kupokelea watalii hali itakayosaidia Kituo hicho kuwa na miundombinu bora ya utalii katika ukanda huo.
Mbali na miundombinu hiyo amesema wataangalia uwezekano wa kulipa fidia kwa wananchi ili kuongeza ukubwa wa eneo litakalotumika kwa ajili ya shughuli za kiutalii kama vile kuanzisha bustani ya wanyamapori hai.
Mhe.Kanyasu amesema mkakati wa Serikali ni kuyafanya Maonesho hayo yawe ya kudumu na yenye hadhi ya kitaifa ambapo baada ya Halmashauri kulipima eneo hilo Taasisi za Wizara zitashiriki katika uwekaji wa miundombinu hiyo.
Aidha, Amesema Kwa uwepo wa Kimondo hicho ni fursa kwa wananchi kuweza kujipatia kipato kufuatia watalii kutembelea kituo hicho.
Amesema Wizara yake imelikabidhi eneo hilo la Kimondo kwa Mamlaka ya Eneo la Ngorogoro( NCAA) ili kuchagiza utalii na jukumu la msingi la NCAA ni kuhakikisha wanatengeneza miundombinu bora kwa ajili ya Utalii.
Tunataka eneo hili la Kimondo, Mtalii yeyote atayefika aweze kuona ngoma za asili pamoja na vitu vingine vya kiutamaduni vitakavyomvutia ili aweze kuona kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Nicodemus Mwenga mesema wamejipanga ipasavyo kuhamasisha jamii kuanza kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio Nyanda za Kusini.
Katika Maadhimisho hayo Wakuu wa mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini pamoja na Makatibu Tawala wameungana kwa pamoja kutangaza vivutio vya utalii Kwa pamoja.