Serikali imefuta kesi 70 zilizokuwa zinawakabili watuhumiwa mbalimbali waliokuwa kwenye gereza Kuu la Butimba ikiwepo kesi namba moja ya uhujumu uchumi namba moja ya mwaka 2019 ya utoroshaji wa dhahabu inayowakabili askari Polisi wanane mkoani Mwanza.

Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustino Mahiga, amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza, leo Jumatano baada ya kutembelea magereza ya kanda ya Ziwa, ambapo katika Gereza la Butimba amekuta na mahabusu waliokaa kwa miaka mitano kutokana na upelelezi wa shauri kutokamilika.