Kila mwaka ifikapo tarehe 7 ya mwezi Julai watanzania tunasherehekea kilele cha maonyesho ya biashara ya SabaSaba. Siku ya Sabasaba hapo awali ilikuwa ni kwa ajili ya kuadhimisha kuanzishwa kwa Chama cha TANU kilichoipatia uhuru Tanganyika.

Siku zinavyozidi kwenda maonyesho haya yanazidi kuwa na mvuto zaidi kwani ubunifu unaongezeka na washiriki pamoja na wanunuzi ama watazamaji wanaongezeka kila mwaka. Maonyesho hayo hufanyika kila mwaka katika viwanja vya SabaSaba vilivyopo Kurasini jijini Dar es Salaam na kwa sasa yapo chini ya TANTRADE. 

Maonyesho hayo yanahusisha zaidi ya wafanyabiashara 4000 ambao huonyesha bidhaa zao kutoka nyanja mbalimbali kuanzia kilimo-biashara, afya, vifaa vya viwandani, vifaa vya nyumbani, huduma za kibenki na elimu. Zaidi ya mataifa 30 yanashiriki katika maonyesho hayo kila mwaka na watu takriban 400,000 hufika kutembelea viwanja hivyo, na kufanya hilo kuwa soko kubwa sana kwa watangazaji wa biashara.

Katika banda la StarTimes mwaka huu walileta bidhaa mpya kabisa ambayo ni mtambo wa Solar ya kisasa kabisa inayokuja na luninga ya kisasa ya kidigitali yenye king’amuzi ndani.
“Mwaka huu ni tofauti na miaka mingine kwetu kwa sababu kwa mara ya kwanza tunatambulisha bidhaa yetu mpya ya Solar. Inakuja na TV ya kidigitali ambayo mteja wetu atatazama chaneli zote kwa miaka miwili bure kabisa.” David Kisaka Meneja Mauzo StarTimes Kanda ya Pwani.

“Bidhaa ya Solar pamoja na ving’amuzi vya StarTimes na luninga za kidigitali za StarTimes vinaendelea kupatikana kwenye maduka na ofisi za StarTimes hata baada ya Sabasaba kuisha, hivyo ni nafasi ya kujiunga na ulimwengu wa kidigitali hasa msimu mpya wa soka unapokaribia kuanza.” Samwel Gisayi, Afisa Mahusiano StarTimes.
 Mwakilishi wa Idara ya Mauzo, Vitus Lugulumu akitoa maelezo kwa Waziri wa Ulinzi Mhe. Hussein Mwinyi alipotembelea banda la StarTimes kujionea bidhaa mpya ya Solar iliyotambulishwa mwaka huu.
Msanii wa vichekesho Ebitoke akihudumia wateja katika banda la StarTimes, SabaSaba.