Mkali wa sauti kwa upande wa wasanii wa kike kutoka kiwanda cha BongoFleva hapa nchini Tanzania Ruby, ameeleza sababu ya kumuonyesha na kumtangaza mpenzi wake "Kusah" mbele za watu.

Ruby ameeleza hayo baada ya kuulizwa kuhusu kumuonyesha waziwazi mpenzi wake huyo tofauti na alivyokuwa awali baada ya kuwa msiri sana kwenye suala la mahusiano.

"Kila jambo na wakati wake, na mahusiano ambayo wewe mwenyewe ndio unajua yako vipi kwake, haihitaji kuwaonyesha watu, ila inatakiwa kama unafanya basi unafanya kweli kutoka moyoni mwako na kwa mapenzi ya kweli'', amesema.

Aidha mpenzi wake Ruby "Kusah" amedokeza kuwa kwa sasa wamefunga ndoa ya siri kwa kusema "usikute tayari tumeshafunga ndoa, lakini hata sisi tuna mambo yetu binafsi sio kila mtu ajue vitu vyetu, kwa hiyo usikute ndoa ishafungwa na kama bado hawajaona, huenda wakaona hivi karibuni".