MWIGIZAJI mkubwa Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ametamba kuwa, mwanaye wa kiume, Jayden aliyezaa na mwigizaji Chuchu Hans anamfanya kutembea kifua mbele kwani amempa chapa na heshima.  Akichonga na Shusha Pumzi, Ray alisema mtoto wake huyo amempa alama isiyofutika na kuna wakati mwingine anatoa machozi ya furaha kutokana na cheo cha ubaba alichompa.

“Hivi unajisikiaje mtoto wako umezaa anafanana na wewe kila kitu? Kingine mwanangu amenipa heshima ambayo sijaipata miaka yote. Kiukweli Jayden wangu amenipiga chapa ya ushujaa,” alisema Ray.