MUIGIZAJI wa filamu Bongo, Rammy Galis amefunguka kuwa kwa sasa ameamua kuyapa kisogo mambo yote yaliyowahi kumuumiza kwenye maisha yake kwani hayana nafasi kwake kwa sababu hataki kurudi kwenye ukurasa wa maumivu ambao alishausoma. Akichonga na Shusha Pumzi, Rammy alisema kuwa hakuna kitu kizuri kama kuyatupilia mbali mambo ambayo yalishawahi ‘kuvunjavunja’ moyo wako na kusonga mbele kwani utapata nafasi ya kuanza maisha mapya yenye furaha.

“Ninachoamini na niwaambie watu wengine ni kwamba usipopenda kurudi kwenye kurasa ulizosoma yaani ambazo zimewahi kukupa maumivu basi unaweza kusonga mbele kwa haraka sana lakini ukiwa mtu wa kukumbuka tu maumivu itakusumbua sana na hautaweza kusonga mbele,” alisema Rammy bila kuyaanika mambo mbalimbali yaliyowahi kumuumiza maishani.