Rais mwenye umri mkubwa kuliko marais wote ulimwenguni 'Beji Caid Essebsi' amefariki dunia. Ni rais wa nchi ya Tunisia ambaye jana alikimbizwa hospitali kutokana na matatizo ya kiafya na hatimaye kufariki leo akiwa na umri wa miaka 92.

Beji Caïd Essebsi, alikuwa ndiye rais wa kwanza kuchaguliwa nchini Tunisia katika mfumo wa vyama vingi tangu taifa hilo lilipopata uhuru wake mwaka 1956.

Alishika urais huo mwaka 2014 baada ya mtangulizi wake, Zine-el-Abedine Ben kuondolewa madarakani mwaka 2011 baada ya kukaa madarakani kwa miaka 23.