Rais wa Uganda, Yoweri Museveni wa Uganda amewatunukia wachezaji wa timu ya Uganda Cranes dola milioni moja kwa kufuzu kwa raundi ya pili ya michuano ya AFCON 2019 inayoendelea huko Misri.

Museveni alikialika kikosi cha Cranes kikiongozwa na kipa Denis Onyango baada ya kocha wao Sebastien Desabre kujiuzulu na kujiunga na klabu ya Pyramids ya Misri.