Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametemebelea Banda la TIB ‘Group’ lililopo katika viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere na kujionea shughuli za uzalishaji na usindikaji wa nyama za kuku na mayai zinazofanywa na kampuni ya kizalendo ya Mkuza Chicks.

Mkuza Chicks ni mmoja wa wawekezaji wazalendo waliyowezeshwa na Benki ya Maendeleo ya TIB.

Akiwa katika banda hilo Dkt. Kikwete alipatiwa maelezo ya namna ambavyo kampuni hiyo inavyozalisha vifaranga pamoja na usindikaji wa nyama za kuku na kusambaza katika soko la ndani ya nchini.

Akiwa katika banda hilo, Dkt. Kikwete aliahidi kutembelea shamba la Mkuza lilipo Kwalla, Kibaha vijijini ili aweze kujifunza shughuli za ufugaji.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akizungumza na Meneja Masoko wa kampuni ya kizalendo ya Mkuza Chicks, Bw. Howard Ringo (kulia). Katikati ni Mtalaamu wa Mifugo wa Kampuni hiyo, Bw. Malambugi Ahobokile.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akifurahi jambo na wafanyakazi wa Benki ya TIB ‘Group’, ambao ni Meneja Masoko na Uhusiano, Bw. Saidi Mkabakuli (katikati) na Afisa Huduma kwa Wateja, Bi. Praise Eliya (kulia).
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini daftari la wageni wakati alipotembelea Banda la TIB ‘Group’ wakati wa Maonesho 43 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.