Rais John Magufuli ametoa gunia 15 za mchele na ng'ombe watatu kwa wafungwa wa Gereza Kuu la
Butimba mkoani Mwanza.

Hii leo Rais Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Butimba Mkoani Mwanza na
kusikiliza kero za Wafungwa.

‘’Kwa maaskari Magereza nimesikia kilio chenu ninyi hamna tofauti na majeshi mengine na hamuwezi mkawa mnafanya kazi kwa kulalamika, hakikisheni hawa wafungwa hawaingii na simu gerezani, nyembe, wanaofanya biashara na hawa wafungwa wasifanye.” amesema Rais Magufuli.