Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.  John Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa kampuni za Said Salim Bakhresa kufuatia vifo vya wafanyakazi watano wa Azam Media waliopoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea leo tarehe 08 Julai, 2019 eneo la Kizonzo.