Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda amesema kuwa suala la Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kutawala kwa mihula miwili halina mjadala.

Pinda amesema kuwa watu wasiumize kichwa katika hilo"Tusijihangaishe vichwa, ana miaka mitano, na ana miaka mingine mitano.

"Kwamba 2020 kuna mtu anajitokeza wala msihangaishe kichwa, msihangaishe vichwa kwenye eneo hilo ana miaka mitano na ana miaka mingine mitano, mimi nimefanya na baba wa Taifa miaka 8, mzee mwinyi 10, Mkapa 10 kwa nafasi mbili na Kikwete miaka 10," alisema Mizengo Pinda.

"Kwahiyo na mimi nimo nikisema ana anamaliza miaka yake 10 nina nina uhakika na sitashangaa akimaliza miaka 10 mkasema mzee huyu angendelea."