Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Muigai Kenyatta keshokutwa Ijumaa July 5, 2019 atafanya ziara binafsi ya siku 2 hapa nchini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais Kenyatta atatua katika uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita saa 4:00 asubuhi na kisha kuelekea nyumbani kwa Rais Magufuli katika kijiji cha Mlimani Wilayani Chato.

Akiwa Chato, Rais Kenyatta atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli.