Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe akizungumza na wanahabari kuwaelimisha juu ya uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa umeme wa Rufiji unaotarajiiwa kuzinduliwa na Mheshimiwa Rais Dkt John Magufuli Julai 26, 2019. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wanahabari katika ofisi za Mkoa wa Morogoro kuwaelezea juu ya uzinduzi wa mradi wa Umeme wa Rufiji unaotarajia kuzinduliwa July 26, 2019 na Mheshimiwa Raise Dkt John Magufuli. Pembeni kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe na kulia ni msemaji wa serikali Dkt Hassan Abas. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi wa kuzalisha na kufua umeme katika maporomoko ya maji ya Rufiji unaotarajiwa kuzalisha umeme wa mega wati 2115.

Akizungumza na wanahabari mkoani Morogoro juu ya ujio wa Rais Dkt John Magufuli, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amesema kuwa zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi linarajiwa kufanyika Julai 26 mwaka huu ambapo afafanua uwekaji wa jiwe hilo utakuwa chachu ya kuongeza kasi ya ujezi mradi huo ambao kwa sasa ujenzi wake umefikia asilimia kumi na tano kwa kipindi cha miezi nane.

Waziri Kalemani ameongeza kuwa miongoni mwa fursa za moja kwa moja ambazo zimepatika tangu kuanza kwa mradi huo ni pamoja na upatikanaji wa ajira kwa Watanzania sambamba na uwekaji wa umeme katika baadhi ya vijiji vya karibu na mradi kutoka katika mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt.Kebwe Stephen Kebwe amewaomba wananchi kujitokeza na kuendelea kulinda wale watakaojitokeza kuhujumu miundo mbinu huku wakichangamkia fursa ya kuwekeza maeneo husika.

"Niwaombe wakazi wa Mkoa wa Morogoro na Pwani tujitokeze kwa wingi kushuhudia uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa umeme utakaokuwa ni hisitoria ya pekee," amesema.