*Yajizatiti kuzidi kuendelea kuifanyia kazi tuzo waliyoipata katika maonesho ya 43 ya biashara(Sabasaba).


MKURUGENZI wa fedha na utawala wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi (PSPTB) Paul Bilabaye amesema kuwa katika maonesho ya 43 ya biashara (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam  wamezindua rasmi huduma kwa njia ya mtandao ambapo watumiaji watatumia simu za mkononi pamoja na kompyuta zilizounganishwa na intaneti ili kupata huduma za Bodi hiyo.


Amesema kuwa mfumo huo wa kidijitali utarahisisha huduma kwa watumiaji ikiwemo kuokoa gharama na muda sambamba na kuwafikia watumiaji wengi zaidi kwa wakati mmoja.

"Tumeanza rasmi na huduma za mafunzo ambapo wiki chache kutakuwa na warsha ya mafunzo ya tafiti kwa wanafunzi ambao wanamaliza mitihani ya kitaaluma ambapo sasa maombi yote yataombwa kupitia tovuti ya Bodi hiyo"


Aidha amesema kuwa katika maonesho hayo wameshinda tuzo ya Taasisi bora ya udhibiti na kushika nafasi ya tatu jambo ambalo linawapa nguvu na ari katika utendaji kazi zaidi katika kuwahudumia wananchi.


Bilabaye amesema kuwa ushiriki wao katika maonesho haya ya 43 ya Sabasaba kwao yamewapa funzo kubwa, na wamewahudumia wananchi katika huduma zote zinazotolewa na Bodi na hiyo ni kuanzia usajili wa wataalamu, kutoa elimu kuhusiana na mitihani pamoja na na kutatua kero mbalimbali wanazokumbana nao.


Ameeleza kuwa huduma zinazotolewa na Bodi hiyo imekuwa inawaaminisha wananchi na ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Joseph Magufuli kwa utendaji kazi uliotukuka pamoja na kuwaamini wao katika kusimamia taasisi hiyo ya umma.

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa utoaji wa huduma mbalimbali za PSPTB kwa njia ya mtandao tofauti na awali zilikuwa zikitolewa moja kwa moja kutoka ofisza  za Bodi ya PSPTB.
Kuzinduliwa kwa mfumo huo wa kidijitali utarahisisha utoaji wa huduma kwa wadau wote wa PSPTB kwa haraka na ufanisi zaidi na kwa watunwengi.
Afisa mwandamiza Masoko na mahusiano kwa Umma wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na Ugavi (PSPTB), Shamim Mdee(katikai) akitoa ufafanuiz kwa mwananchi aliyetembelea banda la Bodi hiyo kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Mitihani kutoka PSPTB, Philipo Kibona.
 Afisa mwanadamizi wa Huduma za wanachana wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na Ugavi (PSPTB), Martha Mapalala akitoa ufafanuzi kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo kwa Leah Mwakabungu kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Kijana Idrisa Mtinangi(wa pili kushoto) akiuliza swali kwa maofisa wa PSPTB alipotembelea banda leo  kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa Mipango ( PSPTB), James Maghori(wa pili kulia) akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyokuwa yanaulizwa na vijana waliofika katika banda la Bodi hiyo kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.  Wa kwanza kulia ni Mratibu wa Mitihani kutoka PSPTB, Philipo Kibona.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala PSPTB, Paul Bilabaye akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa bodi hiyo katika banda lao kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.  Wa kwanza kulia ni Mratibu wa Mitihani kutoka PSPTB, Philipo Kibona.