MAMBO vipi mpenzi msomaji wangu wa safu hii ya My Style, kama ilivyo kawaida tunakulea mastaa mbalimbali kisha wanaelezea namna wanavyoishi kuanzia mavazi wananayovaa mpaka vyakula wanavyopendelea.  Wiki hii tunaye mwanamitindo Jacqueline Obeid ‘Poshy Queen’ ambaye jina lake lilipata umaarufu kutokana na umbo lake matata alilojaliwa na Mwenyezi Mungu, ungani naye hapa chini:


My Style: Msomaji wangu angependa kufahamu hivi wewe huwa unalala na kuamka saa ngapi?

Poshy: Mimi kama sina kazi yoyote kwa kweli napenda sana kulala, saa tatu niwe nimeshapanda kitandani na kuamka naamka sana saa 12 alfajiri.

My Style: Unapendelea kunywa chai au kitu gani unapoamka na vipi kuhusu mlo wako wa mchana na usiku?

Poshy: Mimi sio mpenzi wa chai kabisa ila kama nikipata juisi asubuhi ninakuwa nimeridhika kabisa na kuhusu mchana sichagui sana ila napenda chakula kizuri cha afya.

My Style: Tuje kwenye upande wa mavazi yana kugharimu kiasi gani?


Poshy: Mavazi hayana vitu vingi lakini napenda kuvaa vitu ambavyo vina ubora wa kutosha, kwa mfano nikibeba begi ni begi la ukweli ila ninachoshukuru mwili wangu hauhitaji vitu vingi nikivaa chochote simpo unakubali tu.

My Style: Na gharama unayotumia katika mavazi yako na hata manukato unayotumia ni kiasi gani?

Poshy: Naweza kuvaa nguo ya kawaida tu lakini gharama yake inaanzia laki mbili na kuendelea, kuhusiana na pafyumu ninapendelea za kupoa lakini nzuri kuanzia laki tatu mpaka milioni moja ambayo inaitwa Mason.

My Style: Watu wengi wana wasiwasi na umbo lako wanadai kuna kitu umefanya vipi kuhusu hilo?

Poshy: Unajua kila mtu wa pembeni anaweza kukuongela vyovyote kwa sababu hakujui lakini wanaokujua wananyamaza, sasa watu kama hao ni wa kuwaangalia tu maana kuna wengine wanajifurahisha tu.

My Style: Unaepukana vipi na usumbufu kutoka kwa wanaume mbalimbali kutokana na umbo ulilo nalo?

Poshy: Usumbufu upo kwa kila mwanamke ni jinsi tu ya kukabiliana nao na pia kuongea kistaarabu kwa anayekusumbua kwa sababu mwisho wa siku lazima wewe ni wa mtu maalumu aliyepangwa kwa ajili yako.

My Style: Vipi kuhusu duka lako la Poshy Secret, bado lipo au umeachana na biashara kwa sasa?

Poshy: Lipo na tunaendelea kuuza vitu vizuri vya wadada na wakina kaka zetu wanaojipenda.

My Style: Kwa nini uliamua kufungua duka linalouza nguo za ndani na sio vitu vingine kama nywele na vipodozi mbalimbali?


Poshy: Mimi ninachoamini ni kwamba hakuna kitu kizuri kwenye mwili kama kuwa na nguo za ndani nadhifu ni fahari na mimi ndivyo ninapenda nikaona bora nifungue hiki kitu.

My Style: Wanawake wengi wanapenda sana nywele lakini wewe mara nyingi sikuoni na nywele ndefu kama walivyo wanawake mastaa mbalimbali hapa kwetu ni kwa nini labda.

Poshy: Sio mpenzi sana wa nywele labda itokee tu nivae lakini napenda nywele fupi zilizokatwa Bob Style.

My Style: Haya asante sana Poshy.

Poshy: Asante sana.