Polisi nchini Brazil wametangaza taarifa rasmi kuhusiana na tuhuma za ubakaji zilizokuwa zinamkabili mshambuliaji wa PSG Neymar, polisi nchini humo leo wametangaza kufuta kesi hiyo kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha licha ya uchunguzi kufanyika.

Waendesha mashitaka nchini Brazil wanasiku 15 za kujiridhisha na tuhuma hizo kabla ya jaji kutoa uamuzi wa kesi kusikilizwa au kufutwa rasmi na Mahakama, mwanamitindo wa kibrazil Najila Trindade alimtuhumu Neymar kumbaka wakiwa hotelini nchini Ufaransa mwezi Mei.

Hata hivyo mapema kabisa baada ya kuanza kwa taarifa za tuhuma hizo, Neymar alikana tuhuma hizo za kumbaka mwanamitindo huyo na kusema kuwa ilikuwa ni idhini ya Najila Trindade ambaye ameonekana kugeuka na kufungua kesi kuwa kabakwa.