Kikosi cha Mabingwa wa soka Tanzania, Simba SC, kinaondoka asububi hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar Es Salaam, kuelekea nchini Afrika Kusini, ambako kitaweka kambi ya Maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2019/2020.