Licha ya kuacha shule akiwa na miaka 15, na kujikita kujifunza mchezo wa ndondi, Bingwa wa ndondi Keith Thurman atakutana uso kwa uso na mkongwe Manny Pacquiao Jumamosi Julai 20 katika ukumbi wa bustani wa Grabd jijini Las Vegas Marekani.

Pambano linatazamiwa kuwa kali na la aina yake kutokana na kasi na uzito wa ngumi za Thurman zitakutana na ujuzi na uzoefu wa Pacquiao.

Kocha wa Manny Pacquiao Freddie Roach amesema, pambano hilo litakuwa la kipekee kutokana na mabondia wote kuwa na kasi wanapokuwa ulingoni huku akiamini Manny ataenda kumpiga Thurman