Mkurungezi Mkuu wa Kampuni ya Nikkyo Japanese Leon Sera(kulia) inayojihusisha na uuzaji wa magari kwa njia ya mtandao akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo nchini Tanzania.Lengo ni kurahisisha watanzania kuagiza magari kupitia kampuni hiyo kwa gharama nafuu kwa magari yenye ubora.Katikati ni Meneja mkazi nchini Tanzania wa kampuni hiyo Abbas Mussa na kushoto ni mmoja wa maofisa wa Nikkyo barani Afrika KentaroIkezawa.
Meneja Usafirishaji wa NIkkyo nchini Tanzania Aaliyah Abdulrhman akifafanua kwa kina kwa wageni waalikwa kuhusu ambavyo wamejipanga kuhakikisha wateja wao wanapata magari yaliyo bora.Ametoa ombi kwa Watanzania kuitumia Nikkyo kuagiza magari pindi.
Mkurugenzi Mkaazi wa kampuni ya Nikkyo nchini Tanzania Pili Mkufunzi akizungumza ujio wa kampuni hiyo ambayo ilishaingia nchini mwaka mmoja uliopita na sasa imetangazwa rasmi na kuomba Watanzania kuitumia katika kuagiza magari ya aina mbalimbali kutoka Japan.
Viongozi wa kampuni ya Nikkyo wa nchini Tanzania na Japan wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuizindua rasmi kampuni hiyo ambayo inajihusisha na uuzaji wa magari kwa njia ya mtandao.Utambulisho umefanyika jijini Dar es Sala na kuhudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali.
Meneja Masoko mkaazi wa kampuni ya Nikkyo nchini Tanzania Abbas Muusa akizungumza wakati wa sherehe za kuitambulisha kampuni hiyo kwa Watanzania ambayo ina uzoefu katika biashara hiyo kwa miaka 24 na kwa Tanzania imeingia mwaka jana.

Na Mwandishi Wetu.

KAMPUNI ya uagizaji, usafirishaji na uuzaji magari ya nchini Japan ‘Nikkyo’ imeingia na kuwekeza katika biashara hiyo nchini huku ikiahidi kutekeleza kwa vitendo adhma ya Serikali katika kukuza uchumi kupitia mpango wake wa maendeleo ya viwanda.

Aidha katika kutekeleza adhma hiyo, Kampuni hiyo iliyoanzishwa Mwaka 1995 na kufanya uwekezaji katika nchi mbalimbali zikiwemo za Uganda na Kenya imewahikikishia wananchi kuwapa huduma bora na zinazokidhi viwango ili kuendana na malengo iliyoyakusudia.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shughuli za kampuni hiyo hapa nchini Mkurugenzi Mtendaji wa Nikkyo Leon Sera alisema kuzinduliwa kwa kampuni hiyo hapa nchini ni mkakati unaolenga kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwaletea maendeleo wananchi kupitia sekta ya usafirishaji.

Alisema katika kutekeleza mkakati huo Nikkyo ambayo ina ubobezi wa zaidi ya miaka 20 katika sekta ya uuzaji magari, imejipanga kuwafikia wananchi wenye mahitaji ya ununuzi wa magari ya aina mbalimbali kutoka nchini Japan na kuwafikishia pasipo usumbufu wowote.

“Tumeingia kuwekeza hapa nchini kutokana na uwepo wa mazingira mazuri na kuvutia uwekezaji, kwetu ni fahari kubwa kuja kuwekeza katika Taifa hili ambalo kwa sasa limejielekeza katika kukuza uchumi wake kupitia viwanda, tuna ahidi kuwa tutafanya shughuli zetu kwa uaminifu mkubwa” alisema Sera.

Alisema kampuni hiyo ambayo inauza magari hayo kupitia mtandao kwa mteja kuchagua aina ya gari anayoihitaji, inampa uhahika mteja wa kupata gari analolihitaji likiwa salama na lenye ubora kwa lengo la kutimiza matakwa ya mteja huyo.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni hiyo tawi la Tanzania Abbas Ally, alisema ujio wa kampuni hiyo hapa nchini kutawawezesha watu wenye mahitaji kuondokana na usumbufu waliokuwa wakiupata katika uagizaji magari.

Alisema ukitifautisha na kampuni nyingine zinazojishughulisha na uuzaji wa magari, Nikko imejiwekea utaratibu mzuri wa kutuma mtu kwenda hadi nchini Japan kulikagua gari linalopendekezwa na mteja kabla ya kumletea hapa nchini hatua iliyolenga kumpatia gari iliyo na ubora.

Wakati huo huo Meneja Usafirishaji wa Nikkyo nchini Tanzania Aaliyah Abdulrhman alisema wao wanachoangalia zaidi ni kuhakikisha mteja anayehitaji kuagiza gari kupitiakwao anapata gari yenye uhakika na iliyobora kwani kabla ya kuagiza gari wanatuma maofisa wao kwa ajili ya kufanya uchunguzi na baada ya kuridhika ndipo sasa wanamletea mteja wao.

"Hatuangalii fedha bali kwetu cha kwanza ni ubora wa gari, tunataka kuhakikisha gari inayoagizwa kupitia kampuni yetu inakuwa katika mazingira mazuri na iwapo tutaona kuna tatizo tunamshauri mteja na sio tu kuchukua fedha yake.Tunaomba Watanzania wote wanapotaka kuagiza magari watuitumie Nikkyo kwani inayo uzoefu wa kutosha na kwa Tanzania ndio imeingia lakini katika nchi nyingine barani Afrika na Ulaya imekuwa ikifahamika na maarufu kwa uagizaji magari kutoka Japan,"amesema.