Msanii mwenye uraia wa nchi ya DR Congo anayeishi Tanzania kwa kazi na makazi, Christian Bella, amefunguka ishu zinazomfanya asichukue Uraia wa kuishi Tanzania moja kwa moja.

Kwenye moja ya Interview yake Bella amesema "Nimeishi hapa kwa makazi na kazi, sijachukua kibali cha kuishi moja kwa moja, Vigezo ninavyo vya kupata uraia muda ukifika nitapata tu kwa sababu muda ambao nimekaa naruhusiwa kupata kibali na bado sijafikiria muda wa kuamua kupata Uraia"

Aidha msanii huyo amesema hawezi kutaja kiasi cha pesa anacholipa ili kuishi Tanzania ila ameeleza analipa pesa nyingi sana kila baada ya miaka miwili au mitatu ili kuishi hapa Tanzania kwa sababu amepewa kibali cha juu 'Class A' kwa kuwa anamiliki biashara, kampuni, bendi na studio