Msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda ameeleza namna alivyofanikiwa kugundua kipaji cha kuimba kutoka kwa mpenzi wa rafiki yake wa karibu.

Mziwanda ambaye anatamba na ngoma ya 'Natapatapa' amesema hayo katika kipindi cha Friday Night Live (FNL), alipoulizwa namna alivyogundua kipaji cha msanii mpya wa lebo yake aitwaye Bi Aisha, ambaye alimleta kutambulisha nyimbo yake.

"Kuna stori ndefu sana ya mimi hadi kufahamiana naye na kugundua kipaji chake, 'short and clear' huyu alikuwa ni girlfriend wa rafiki yangu lakini nilikuwa sijui kama huyu ana uwezo wa kuimba", amesema Mziwanda.

"Siku moja nilikwenda kwa rafiki yangu, nikamkuta ana 'mike' anafanya Kareoke ndani mwake, nilipofungua studio nikamchukua", ameongeza.