Ndege maalum ya Jeshi la Kenya iliyobeba Dhahabu ya Tanzania iliyokamatwa Kenya ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kabla ya kukabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli atashuhudia makabidhiano hayo Ikulu Dar es Salaam kutoka kwa Mjumbe Malalum wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyata.