Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imesema kuwa wanaohitaji kufanya mitihani ya Bodi usajili umeanza sasa.

Akizungumza katika maonesho ya elimu ya Vyuo Vikuu katika viwanja vya Mnazi Mmoja Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA Magreth Kageya amesema kuwa mithani hiyo inatarajiwa kufanyika  mwezi Novemba mwaka huu.

NBAA inashiriki maonesho ya Vyuo Vikuu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ili kuonesha huduma mbalimbali zinazotolewa na Bodi hiyo pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi waliofika kwenye banda la Bodi hiyo.

Baadhi ya huduma zinazotolewa na NBAA katika kipindi hiki cha maonesho ya Vyuo Vikuu ni Usajili wa Wanafunzi ili kuweza kufanya mitihani ya Bodi hiyo kwa ngazi mbalimbali  kuanzia ngazi ya chini (Accounting Technician)  mpaka  ile ya Taaluma (Profession) pamoja na usajili wa wanachama  na makampuni ya kihasibu na Kikaguzi.

"Tumedhamiria kutoa huduma zetu kiurahisi kwa wale wanaofanya mitahani ya Bodi na wanachama wetu ili waweze kutambulika na Taasisi mbalimbali katika umahiri wa kazi za Kihasibu na Kikaguzi" amesema Kageya 
Afisa Msaidizi Idara ya Elimu na Mafunzo, Joachim Luguzye(katikati) akiwaonesha namna wanavyotoa mafunzo pamoja na utoaji wa Mitihani  kwa baadhi ya wananchi waliotembelea Banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Mkaguzi wa Viwango vya Wakaguzi wa Hesabu wa NBAA, CPA Winnington Makaka.
Mwanafunzi Geraldina Tarimo(kulia) akiuliza swali kwa maofisa wa NBAA alipotembelea Banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Afisa Msaidizi Idara ya Elimu na Mafunzo, Joachim Luguzye. na Katikati ni Msaidizi wa Uhasibu wa NBAA, David Iman.
Msaidizi wa Uhasibu wa NBAA, David Iman akitoa maelezo kwa mwanafunzi Geraldina Tarimo(kulia) alipotembelea Banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Msaidizi Idara ya Elimu na Mafunzo, Joachim Luguzye.
Afisa Masoko na Mawasiliano kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Magreth Kageya(wa pili kushoto) akitoa maelezo jinsi Bodi hiyo inavyofaya kazi kwa wanafunzi waliotembelea banda hilo kwenye Maonesho ya Vyuo vikuu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkaguzi wa Viwango vya Wakaguzi wa Hesabu wa NBAA, CPA Winnington Makaka.
Afisa Msaidizi Idara ya Elimu na Mafunzo, Joachim Luguzye(kushoto) akitoa maelezo kuhusu namna mitihani ya Bodi hiyo inavyotolewa pamoja na gharama kwa mwanafunzi Stanley Beli(kulia) alipotembelea Banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 
Mkaguzi wa Viwango vya Wakaguzi wa Hesabu wa NBAA, CPA Winnington Makaka (kushoto) akitoa ufafanuzi namna ya kufanya mitihani ya Bodi hiyo kwa Trypone Richard (kulia) alipotembelea Banda la Bodi ya TaifaA ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 

Afisa Msaidizi Idara ya Elimu na Mafunzo, Joachim Luguzye(katikati) akitoa ufafanuzi kwa mwanafunzi Stanley Beli (kulia) aliyefika kwenye Banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Mkaguzi wa Viwango vya Wakaguzi wa Hesabu wa NBAA, CPA Winnington Makaka.
Msaidizi wa Uhasibu wa NBAA, David Iman  akimsikiliza mwananchi aliyefika kwenye banda la NBAA katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.