Marekani ilikasirishwa na hatua ya Urusi kuipatia Uturuki mfumo wa makombora ya masafa marefu
Muda unakwisha wa kuunusuru mkataba muhimu wa na urusi, katibu Mkuu wa wa muungano wa Nato Jens Stoltenberg amiambia BBC.

Bwana Stoltenberg ameahidi kuwa zitachukuliwa hatua "zilizopangwa na za kujilinda " kama Urusi haitarejea katika utekelezaji wa mkataba ifikapo tarehe 2 Agosti ambao ni muda wa mwisho uliowekwa.

"lazima tujiandae kwa ajili ya dunia... Kutokana na makombora zaidi ya Warusi ," amesema Kiongozi wa Muungano wa kujihami la nchi za magharibi-NATO

makubaliano ya 1987 yaliyosainiwa baoina ya Marekani na Muungano wa Usoviet USSR yalipiga marufuku makombora ya masafa mafupi na marefu.

WHO: Mlipuko wa Ebola janga la dharura
Instagram kuficha idadi ya 'likes' kuondoa 'ushawishi'
Tetesi za usajili Ulaya Alhamisi 18.07.2019
Rais Trump alitangaza kuwa Marekani itaacha utekelezaji wa majukumu yake chini ya mkataba juu ya vikosi vya masafa vya nuklia mwezi Februari, ikiishutumu Urusi kwa kukiuka mkataba huo.

Urusi inakana madai hayo, lakini ilisitisha kwa muda utekelezaji wa majukumu yake ya mkataba huo muda mfupi na baadae kutangaza mipango ya kutengeneza mfumo wa silaha za nuklia.

Haki miliki ya pichaAFP
Image caption
Kiongozi wa Muungano wa Usovieti Mikhail Gorbachev na rais wa Marekani Ronald Reagan walisaini mkataba wa udhibiti wa makombora ya kijeshi mwaka 1987
Katika mahojiano mahojiano ya kina na BBC, Bwana Stoltenberg anasema Makombora ya Urusi - ambayo anasema ni "ukiukaji wa wazi wa mkataba" - yanauwezo wa kinuklia, kutumika popote, ni magumu kuyatambua, na yana uwezo wa kuifikia miji ya Uolaya katika kipindi cha dakika chache.

"Hili ni tatizo kubwa. Mkataba wa udhibiti wa matumizi ya nuklia umekuwa muhimu katika udhibiti wa silaha kwa karne kadhaa na sasa tunashuhudia kukiukwa kwa mkataba," alisema.

Huku kipaumbele kilikuwa nu kuirejesha Urusi kuheshimu kanuni za mkataba , Bwana Stoltenberg amesema ''hakuna ishara zozote " kuwa nchi hiyo itafanya hivyo. "kwa hiyo tunapaswa kujiandaa kwa ajili ya dunia bila makataba wa udhibiti wa silaha na kwa jaili ya makombora zaidi ya Urusi ."

NATO; hatutaki mzozo na Urusi
Huku NATO ikiwa haina mpango wa kupeleka makombora yake nuklia ya ardhini yaliyoko Ulaya, Bwana Stoltenberg amesema kuwa Muungano huo utajibu kwa kiwango " kilichopimwa, kwa njia ya kujilinda" ikiwa Urusi itakataa kurejea katika utekelezwa wa mkataba ifikapo tarehe 2 Agosti.

Makombora ya ulinzi , mafunzo mapya na utayari wa wanajeshi , na udhibiti wa silaha mpya , kwa pamoja vinaweza kuwa ni sehemu ya namna NATO itakavyoingilia kati, alisema. Uamuzi wowote wa mwisho utachukuliwa baada ya muda wa mwisho uliowekwa kwa Urusi kurejea kwenye mkataba.