Christopher Philemon - Uchukuzi
NAIBU Waziri  wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano(Sekta Uchukuzi na Mawasiliano),  Mhandisi Atashasta Nditiye, amesema ujenzi wa jengo la  tatu la abiria wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA),  kinatarajia  kukamilika mwanzoni mwa Agosti  mwaka huu kwa kuanza kuhudumia abiria

 Amesema amefurahishwa  kwa  kukamilika  kwa ujenzi wa kiwanja hicho  ambapo kwa  vimefungwa vifaa vya kisasa.  Akizungumza mara  baada ya ziara ya kukagua kiwanja hilo, amesema  kuwa katika idadi ya miruko ya ndege Barani Afrika  inachukua nafasi ya tano  na nafasi ya sita kwa abiria.

‘’ Nimefurahishwa kwa kukamilika kwa ujenzi wa jengo la tatu la abiria wa  kiwanja cha Ndege ambapo utakapoanza kuhudumia abiria natarajia tutachukua nafasi mzuri zaidi Barani Afrika kwani ni kiwanja cha kisasa nahuduma zetu ni mzuri,’’ alisema.

Nae Mkurugenzi  wa Kiwanja cha Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere( JNIA),  Paul  Rwegasha, amesema  kukamilika kwa jengo hilo litaweza  kuhudumia  jumla abiria milioni nane kwa mwaka.
Rwegesha alisema  ujenzi wa jengo la kwanza lina uwezo wa kuhudumia abiria 500,000 kwa mwaka na ujenzi wa pili abiria  milioni 1.5

Alisema kukamilika kwa Jengo la tatu la abiria  litaongeza idadi ya ndege, abiria pamoja na watalii baada ya kuwa na miundombinu  bora na yakisasa. Vile vile alisema ujenzi wa kiwanja cha tatu ni kwa ajili ya abiria wa safari za Kimataifa ambapo kwa sasa yako mashirika na Kampuni 20 na kiwanja cha  pili kwa ajili ya abiria wa safari za   ndani ya nchi na Kimataifa  ambapo yana Kampuni sita  huku kiwanja cha kwanza  safari za  ujumla za ndani ya nchi Kampuni ni  12.

Alisema ujenzi wa jengo la tatu la abiria  litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 2,800, kwa saa na maegesho ya magari mchanganyiko yasiopungua 2,075 kwa wakati mmoja. Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini(TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama, alisema wako katika maandalizi ya wakuu wanchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa 39 wa SADAC  ambapo maadalizi yameambatana na ukarabati wa maboresho ya miundombinu  na samani katiaka jengo  la pili la Abiria.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka wa Viwanja vya Ndege Tanzania Mhandisi Julius Ndyamukama (mwenye koti jeusi)akisoma Taarifa ya Mradi wa Jengo la III la abiria kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye alipofanya ziara katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere mapema leo.
 Msimamizi wa jengo la III la abiria Mhandisi Barton Komba (aliesimama mbele) akitoa maelezo ya eneo la kuondokea la watu mashuhuri kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye alipofanya ziara katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere mapema leo.
 Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye akihoji jambo katika Ukumbi wa Watu mashuhuri alipotembelea jengo la III la abiria mapema leo.
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Bw, Paul Rwegasha ( mwenye koti kijivu) Akitoa maelezo ya jengo la mizigo linalokarabatiwa kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye wakati alipofanya ziara katika Kiwanja hicho mapema leo.