Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na Waoneshaji kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Utalii wa Utamaduni ya Serengeti yanayofanyika wilayani Serengeti mkoani Mara. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akiwa na pamoja na viongozi wengine.
Naibu Waziri wa Malasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (wa kwanza kushoto) akiwa na Mbunge wa Serengeti, Mhe.Chacha Ryoba ( katikati) wakipewa maelezo na muuza vinyago ambaye ni miongoni mwa Washiriki wa Maonesho hayo ya Utalii wa Kiutamaduni huku akiwa ameshika kinyago alipokuwa akimuelezea ubora wa Kinyago hicho katika Maonesho ya Utalii wa Utamaduni ya Serengeti yaliyofunguliwa rasmi mkoani Mara. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Maonesho hayo, Joshua Nyansiri.
Naibu Waziri wa Malasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa na Mbunge wa Serengeti, Mhe.Chacha Ryoba wakipewa maelezo kuhusu dawa za mitishamba kabla ya kuzindua Maonesho ya Utalii wa Kiutamaduni ya Serengeti.
Naibu Waziri wa Malasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ( katikati) akiwa ameshika fimbo ikiwa ni zawadi aliyokabidhiwa na Mkuu wa kikundi cha Utamaduni, Chacha Sengwa kama ishara ya shukrani ya kukubali kufungua Maonesho ya Utalii wa Utamaduni ya Serengeti mkoani Mara.Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Mhe. Nurdin Babu.
Naibu Waziri wa Malasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ( katikati) akikabidhiwa fimbo ikiwa ni zawadi aliyokabidhiwa na Mkuu wa kikundi cha Utamaduni, Chacha Sengwa kama ishara ya shukrani ya kukubali kufungua Maonesho ya Utalii wa Utamaduni ya Serengeti mkoani Mara.Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Mhe. Nurdin Babu.
Mku wa wilaya ya Serengeti, Mhe. Nurdin Babu akizungumza na Waoneshaji kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Utalii wa Utamaduni ya Serengeti yanayofanyika wilayani Serengeti mkoani Mara kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu kwa ajili ya kufungua maonesho hayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa ameshika pambo ambalo imetengenzwa na Mjasiliamali huku akipewa maelezo na Anna Chengula kabla ya kufungua maonesho hayo.( Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii).

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ameiagiza Hifadhi za Taifa (TANAPA) kupitia upya sheria ya tozo ya kiingilio kwa watalii wanapotoka nje ya Hifadhi inayowalazimu kulipwa tena wanapoingia ndani ya Hifadhi maarufu kwa jina la Single Entry waiondoe kwenye maeneo yanayolalamikiwa kuwa imeua shughuli za Utalii kwenye vijiji vinavyozunguka Hifadhi.

Aidha, Mhe. Kanyasu ameagiza TANAPA iangalie maeneo ambayo inadhani ni muhimu kwa Single Entry iendelee kutumika kuwa waweke mfumo wa kielektroniki wa utambuzi wa vidole ( Biometric Identity) utakaoweza kutumika kubaini udanganyifu endapo utafanyika.

Amesema mfumo huo utawalazimisha watalii kuweka kidole wakati wakiwa wanaingia na wakati wanapotoka nje ya Hifadhi.

Amesema hali hiyo itawasaidia Waongoza watalii kutoka nje ya Hifadhi na Watalii wao kwa ajili kuzitembelea jamii zilizokaribu na Hifadhi na hivyo kuzisaidia jamii kunufaika moja kwa moja kupitia utalii wa kiutamaduni.

Hayo yamesemwa kupitia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakati alipokuwa akifunga Maonesho ya 8 ya Utalii wa Utamaduni ya Serengeti mkoani Mara.

Amesema tangu kuanzishwa kwa Single Entry kumepelekea madhara makubwa kwa baadhi ya maeneo yaliyo karibu na Hifadhi za Taifa kudumaa kiutalii.

Ameyataja maeneo hayo yaliyokaribu na yaliyoathirika moja kwa moja kuwa ni ukanda wa Magharibi katika geti la Ndabaka katika Hifadhi ya Serengeti na katika Hifadhi ya Ruaha.


Akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho hayo, Kanyasu amesema maeneo yaliyoathirika zaidi kutokana na kuwepo kwa Single Entry ni yale maeneo ambayo hayajapitiwa na barabara kuu pamoja na viwanja vya ndege.

Ametaja sababu zilizopelekea kufa kiutalii maeneo hayo kuwa watalii walio wengi hulazimika kukaa ndani ya Hifadhi hadi muda wa masaa 24 yanavyoisha bila kutoka wakikwepa gharama endapo watatoka.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu alimueleza Naibu Waziri huyo kuwa wilaya yake asilimia 80 ni eneo la Hifadhi ya Taifa ya Serengeti hivyo kutokana na uwepo wa Single entry wilaya hivyo imeathirika sana kwa vile imekosa watalii wanaotembelea vijijini tofauti na ilivyokuwa mwanzo kabla ya kuanzishwa.

" Mhe.Waziri tunakuomba uliangalie suala hili, utalii wa kiutamaduni uliosaidia kuajiri wananchi wengi umekufa kutokana na Single Entry" alisisitiza

Ameongeza kuwa endapo itaondolewa itasaidia watalii kuweza kutoka nje ya Hifadhi kuembelea vituo vingi vya utalii ambavyo vipo nje ya Hifadhi.

Naye, Anaeli Kilemi aliyesoma risala mbele ya Waziri huyo amesema Single entry imewadidimiza wananchi wengi ambao walikuwa wamejiajiri kupitia utalii wa kiutamaduni, Hivyo anaiomba serikali itatue tatizo hilo.